Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bulembo awaonya wazazi wanawaficha wanafunzi kidato cha kwanza

Maabara Wanafunzi Bulembo awaonya wazazi wanawaficha wanafunzi kidato cha kwanza

Wed, 18 Jan 2023 Chanzo: mwanachidigital

Jumla ya wanafunzi 3,396 kati ya wanafunzi 4,873 sawa na asilimia 69. 58 wameripoti kuanza masomo ya kidato cha kwanza katika Wilaya ya Muheza huku wanafunzi 1,487 wakiwa hawajaripoti kuanza masomo hayo.

Akizungumza katika ziara yake ya kata kwa kata yenye lengo la kusikiliza na kutatua kero za wananchi pamoja na kukagua miradi ya maendeleo , Mkuu wa Wilaya ya Muheza mkoani Tanga Halima Bulembo amewataka Wazazi na walezi ambao watoto wao hawajaripoti wahakikishe wanawapeleka shule vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Pia amesema watawachukulia hatua kali za kisheria wazazi wote wanaowaficha watoto wenye ulemavu ili wasipate haki yao ya msingi ya kupata elimu. mbili za Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi

Bulembo akiwa kata ya Mhamba amesema kuwa watoto waliochaguliwa kwenda kidato cha kwanza katika kata hiyo ni 53 kati ya hao walioripoti ni 27 na 26 hawajaripoti.

Mkuu huyo wa wilaya yupo katika ziara ya kata Kwa kata ambapo anatarajia kupita katika kata zote 37 zilizopo wilayani humo.

Chanzo: mwanachidigital