Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Breaking: Wawili Wafariki kwa Kugongwa na Treni Morogoro

Treni 2?fit=1280%2C720&ssl=1 Breaking: Wawili Wafariki kwa Kugongwa na Treni Morogoro

Mon, 10 May 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Breaking: Wawili Wafariki kwa Kugongwa na Treni Morogoro May 10, 2021 by Global Publishers



Watu wawili wamepoteza maisha kufuatia ajali iliyohusisha pikipiki ya magurudumu matatu (Bajaj) waliyokuwa wakisafiria na treni katika eneo la Modeko, Kata ya Mazimbu Mkoani Morogoro.



Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo, waliopoteza maisha ni mwanamke aliyetambulika kwa jina moja la Fatuma anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 35, sambamba na dereva wa Bajaj ambaye bado jina lake halijafahamika.



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fortunatus Muslim, amesema amepokea taarifa za awali kuhusu ajali hiyo na kueleza kwamba kwa mujibu wa sheria, Bajaj ndiyo iliyoligonga treni na kuongeza kwamba tayari amewaagiza askari wa usalama barabarani kwa kushirikiana na askari wa Mamlaka ya Reli, kwenda eneo la tukio.



Ameeleza kwamba taarifa kamili kuhusu ajali hiyo, zitatolewa baadaye.
Chanzo: globalpublishers.co.tz