Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Breaking: Mkurugenzi Igunga afariki kwa ajali

Ded Igunga Breaking: Mkurugenzi Igunga afariki kwa ajali

Wed, 14 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Fatuma Omary Latu pamoja na dereva wake leo Jumatano, Septemba 14, 2022 wamefariki dunia eneo la Shamwengo, Inyala mkoani Mbeya.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amethibitisha kutokea vifo hivyo na kueleza kuwa chanzo cha ajali hiyo, ni uzembe wa dereva wa gari la mkurugenzi aliyekaidi amri ya jeshi la polisi kusimama ili kupisha msafara wa malori.

Ajali hiyo imehusisha pia magari mengine mawili, likiwemo lori la mafuta, mali ya kampuni ya Lake Oil na lori lingine la mizigo ambapo pia utingo wa lori la mafuta naye amefariki kwa ajali hiyo.

Imeelezwa kuwa, Mkurugenzi huyo alikuwa anatoka kwenye mkutano wa ALAT.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live