Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Breaking: Lori lasaga magari mawili Tegeta Wazo

Ajali Tegeta Breaking: Ajali yadaiwa kuua watatu Tegeta Wazo

Fri, 11 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu watatu wanasadikiwa kupoteza maisha na mmoja kujeruhiwa baada ya Lori lililokuwa limebeba Saruji kuyagonga magari mawili madogo katika eneo la Tegeta Wazo, Dar es Salaam, leo Ijumaa, Novemba 11, 2022, asubuhi.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, inasemekana lori hilo lilifeli breki na kwenda kuyasaga magari hayo mawili ambayo katika picha yanaonekana yamebondeka vibaya.

Tayari jitihada za uokoaji linaendelea kwa kutumia crane za Kiwanda cha Wazo ili kunasua watu walionasa ndani ya magari hayo na kuyatoa magari.

Taarifa zaidi zitakufikia hivi punde

Chanzo: www.tanzaniaweb.live