Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Breaking: Baraza la Madiwani Lamkataa Mkurugenzi Mbozi

Madiwani?fit=612%2C400&ssl=1 Breaking: Baraza la Madiwani Lamkataa Mkurugenzi Mbozi

Fri, 30 Apr 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

BARAZA la Madiwani katika Halmashauri ya Mbozi kwa pamoja limeazimia kutokuwa na imani na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Hanji Godigodi kutokana madai ya matumizi mabaya ya ofisi ikiwemo upotevu wa zaidi ya Sh milioni 117 za halmashauri hiyo.

Uamuzi huo umetolewa leo Aprili, 30 2021 katika kikao cha Baraza hilo kilichoketi na kujumuisha madiwani wote wa baraza hilo.



Akifunga mjadala huo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mbozi, George Musyani amesema kwa pamoja wamekosa imani naye kutokana na madai ya ubadhirifu wa miradi.

Alisema kuwa mkurugenzi huyo ameshindwa kudhibiti mapato ya kahawa pamoja na kuwadharau watumishi wa Halmashauri hiyo.

“Anadharau hata maagizo ya vikao hata maagizo ya kamati ya fedha.

“Tunaomba mamlaka za nidhamu na teuzi zimuwajibishe na kumuondoa katika Halmashauri hii kwa sababu ameshindwa kusimamia mapato. Pia tunaviomba vyombo uchunguzi kumchunguza iwapo kuna mianya ya rushwa katika mapato ya ushuru wa kahawa,” alisema.

Aidha, akizungumza na Global kuhusu tuhuma hizo Mkurugenzi huyo alisema yupo tayari kufanya kazi bila madiwani hao kwa sababu wanamuongezea gharama za uendeshaji.



“Mimi bado ni mkurugenzi na ninaweza kufanya kazi bila hata hao madiwani… uwepo wao pia ni gharama kwa sababu wanataka nitoe pesa bila utaratibu.

“Kwa sasa nasubiri mamlaka walizoziomba kutoa maamuzi dhidi yangu, ila kwa sasa mimi bado ni mkurugenzi,” alisema.

NA MWANDISHI WETU
Chanzo: globalpublishers.co.tz