Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Boti iliyotengenezwa kwa takataka kupinga uchafuzi Ziwa Victoria

727f2ceda336c96b4c6d7da4813ac30c Boti iliyotengenezwa kwa takataka kupinga uchafuzi Ziwa Victoria

Mon, 12 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SERIKALI mkoani Mwanza, imepokea boti iliyotengenezwa kwa takataka za plastiki zilizokusanywa katika vyanzo vya maji, itakayotumika kupinga uchafuzi kwenye Ziwa Victoria.

Tukio hilo ilikuwa ni sehemu ya uzinduzi wa kampeni ya kupinga uchafuzi kwa plastiki yenye kaulimbiu: “Ziwa Letu, Uchumi Wetu, Kazi Iendelee.” Boti hiyo yenye uzito wa tani 7.5 ilitengenezwa kwa tani 12 za uchafu wa plastiki uliokusanywa kutoka Bahari ya Hindi upande wa Kenya zikiwemo jozi 30,000 za takataka za kandambili.

Ilijengwa mjini Mombasa nchini Kenya na imetumika kufanya kampeni za kupinga uchafuzi katika nchi hiyo na Uganda. Ofisa Usafi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Danford Kamenye, alisema kulinda Ziwa Victoria ni muhimu kwa ustawi wa mamilioni ya watu wanaozunguka na kulitegemea ziwa hilo kiuchumi na kijamii.

“Kampeini hii ni endelevu kwani watu wanaolizunguka ziwa wanaweza kudhurika kwa namna moja au nyingine kwa kuwa utafiti tofauti wa hivi kari umeonesha moja kati ya samaki watano wanaovuliwa katika Ziwa Victoria, ana chembe za plastiki ndani yake,” alisema Kamenye.

Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN), Clara Makenya, alisema kati ya tani 8 hadi 12 za uchafu wa plastiki hutupwa baharini na kuathiri mfumo wa ikolojia. “Kila mmoja katika jamii ana jukumu la kulinda na kutunza maziwa na bahari zetu,” alisistiza.

Chanzo: www.habarileo.co.tz