Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bosi Tanroads asema barabara Morogoro-Dodoma ni chakavu, ina miaka 40

98155 Pic+tanroads Bosi Tanroads asema barabara Morogoro-Dodoma ni chakavu, ina miaka 40

Fri, 6 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro. Wakati meneja wa Tanroads mkoani Morogoro, Godfrey Andalwisye akiondolewa kwa madai ya kutokagua miundombinu, mtendaji mkuu wa taasisi hiyo, Patrick Mfugale amesema barabara ya Morogoro-Dodoma ni chakavu kwa kuwa imejengwa muda mrefu.

Kauli hiyo ya Mfugale imekuja siku moja baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuagiza Andalwisye arudishwe makao makuu kutokana na kutokagua barabara hiyo ambayo daraja lake la Kiyegeya lililoko wilayani Kilosa lilisombwa na maji.

Waziri Mkuu, ambaye juzi alikuwa ameenda eneo hilo kushuhudia ujenzi wa daraja hilo, alishangaa kuona mkoa wenye wahandisi 12, kushindwa kufanya ukaguzi wa barabara na madaraja.

Lakini jana, Mfugale alisema barabara hiyo ilijengwa miaka 40 iliyopita na hivyo imeshatumika muda mrefu ndio maana kila mara wamekuwa wakiifanyia ukarabati.

Alisema kukatika kwa daraja hilo ni jambo la kawaida kiutaalamu kwa kuwa uhai wa makalavati yanayowekwa si zaidi ya miaka 25.

Alisema tayari Serikali iko katika mchakato wa kuijenga upya barabara hiyo na madaraja yake.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement
Pia, alizungumzia mikakati wanayoendelea nayo ya kujenga barabara ya michepuko na kukamilisha daraja hilo ili liweze kupitisha magari sehemu zote mbili, alisema ndani ya wiki moja ujenzi wake utakuwa umekamilika.

Foleni bado

Wakati ukamilishaji ujenzi wa daraja la Kiyegeya ukiendelea, foleni hasa ya malori bado imeendelea kuwa changamoto kwa kuwa barabara hiyo inapitisha magari machache kwa kila upande.

Foleni hiyo ya malori imeonekana kwa pande zote mbili. Upande wa Morogoro - Dodoma umefikia umbali wa kilometa 15 hadi 20 kutoka eneo la Kwambe hadi lilipokatika daraja hilo huku upande wa kutoka Dodoma–Morogoro eneo la Gairo ikiwa kilometa 30 na askari wa usalama barabarani walikuwa wakisimamia magari hayo kupita kwa awamu.

Tanroads, kampuni ya Yapi Markezi wapo eneo hilo wakiendelea na ujenzi wa njia ya mchepuko wakati ujenzi wa daraja ukiendelea.

Akizungumzia namna wanavyokabiliana na foleni jana, kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Fotunatus Muslimu alisema kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa kupitisha kwa utaratibu magari madogo pamoja na mabasi yaliyokuwa yamekwama kwa muda mrefu.

Alisema kipaumbele kikubwa ni mabasi ya abiria, magari ya wagonjwa na yale yanayosafirisha maiti.

Alisema kutokana na kutengenezwa kwa njia moja, wamelazimika kuruhusu magari hamsini kila upande, lakini wameshauri madereva kuendelea kutumia njia mbadala hasa kwa wale wanaotoka Dodoma kupitia Babati mkoani Manyara, Arusha hadi Dar es Salaam na wale wanaotoka Dar es Salaam watumie barabara ya Morogoro-Iringa-Dodoma.

“Kuna njia ya Berega ambayo inatumika na magari madogo hasa yanayosafirishwa kwenda nje ya nchi ambayo si kwa magari makubwa,” alisema.

Muslimu alisema hali ya usalama ni nzuri na kwamba mpaka sasa hakuna ajali yoyote iliyotokea.

Chanzo: mwananchi.co.tz