Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bosi Precision Air amwaga machozi akieleza ajali ilivyotokea

Precision Air Bosi.jpeg Bosi Precision Air amwaga machozi akieleza ajali ilivyotokea

Sun, 6 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni simanzi, hivi ndivyo inavyoweza kuelezwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Precision Air, Patrick Mwanri kufuatia kuanguka kwa ndege ya shirika hilo asubuhi ya leo na kuwepo taarifa za watu watatu kupoteza maisha.

 Mchana wa leo Novemba 6, Mwanri amezungumza na vyombo vya habari akitoa taarifa zinazoendelea kufuatia ajali hiyo huku akieleza kuendelea kwa kazi ya kuokoa waliokuwa ndani ya ndege.

Wakati wote alikuwa akizungumza uso wake ulionekana kujawa na simanzi na alipomaliza kuzungumza alishindwa kuzuia machozi yaliyotiririka kwenye macho yake.

Ametoa kitambaa chake na kufuta machozi mbele ya waandishi wa habari kisha akanyanyuka na kuahidi atatoa taarifa kadiri watakavyozipata kutoka kwa mamlaka husika.

Katika taarifa yake hiyo amesema jitihada za kuwaokoa watu wote walikuwa kwenye ndege hiyo zinaendelea akieleza kuwa lengo ni kuhakikisha wote wanapatikana.

Kulingana na mkurugenzi huyo ndege iliyopata ajali ina uwezo wa kubeba watu 48 na waliokuwa ndani ya ndege wakati ajali inatokea ni abiria 39 akiwemo mtoto mchanga na wafanyakazi wa Precision Air wanne.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live