Bondia maarufu maeneo ya Manzese jijini Dar anayefahamika wa jina la Komi Mjeshi anadaiwa kumuua mkewe wa ndoa aliyefahamika kwa jina la Mama Imani.
Komi Mjeshi anadaiwa kutekeleza mauaji hayo hii jana asubuhi katika nyumba ya kupanga wanayoishi familia hiyo maeneo ya Tipo Top Manzese jijini Dar.
Kwa mujibu wa mashuhuda, chanzo cha mkasa huo inasemekana kuwa ni wivu wa mapenzi.
Imedaiwa kwamba, wawili hao wamekuwa kwenye mgogoro wa kimapenzi kwa muda mrefu kiasi cha kupeana talaka, lakini lakini wiki moja kabla ya tukio hilo kutokea Komi Mjeshi alikwenda kijijini kwa wazazi wa mwanamke huyo alikodhani ndipo alipokwenda baada ya kupeana talaka, lakini alipofika huko akaambiwa Mama Imani hajafika huko na kumlazimu kurudi mjini akiwaza alikokwenda mzazi mwenzake.
Imeelezwa kwamba, juzi mwanamke huyo alifika nyumbani hapo kuchukua vyombo vyake kwa kigezo cha kwenda kupanga chumba sehemu nyingine.
Hata hivyo, inasemekana leo asubuhi alipigiwa simu kuwa anahitajika kwenda kumsuka mtu maeneo hayo na pia alikwenda nyumbani kumsalimia bibi yake ambaye alikuwa akiuguzwa nyumbani hapo ndipo Komi Mjeshi alipomvamia na kuanza kumshambulia kwa kumchoma visu sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia umauti papohapo.
Polisi walifika eneo la tukio na kuuchukua mwili na kwenda kuuhifadhi katika Hospitali ya Muhimbili.