Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bomu lililotegwa NMB Shinyanga, lateguliwa na JWTZ

Bomu Airport Bomu lililotegwa NMB Shinyanga, lateguliwa na JWTZ

Sun, 18 Sep 2022 Chanzo: TheCitizen

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi, amesema Polisi kwa kushirikiana na JWTZ wamefanikiwa kutegua Bomu lililokutwa kwenye chumba maalum kinachotumiwa na wateja wa Fedha nyingi (Bulk) kwenye Benki ya NMB na Mtuhumiwa amekamatwa.

Kwa mujibu wa Kamanda Magomi, Kilipuzi hicho kilipatikana kwenye mkoba uliokutwa na kilipuzi hicho ulisafirishwa hadi Kambarage Police Barracks ambapo wataalam wa Mabomu kutoka JWTZ walifika na kuufyatua kwa haraka.

Tukio hilo lilifanyika Septemba 17 muda wa saa 7 mchana.

Mmoja wa mashuhuda Janeth Ernest alisema mtuhumiwa huyo alikuwa amekaa sehemu ya wateja wa Bulk na alikuwa anajaza fomu za benki, kisha akavua koti na kuliweka kwenye mkoba Baadaye alitoa chupa na kumimina vilivyokuwa ndani ya kanzu kisha kuiwasha na kuondoka eneo la tukio.

Chanzo: TheCitizen