Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bomoabomoa yaja waliovamia kiwanda cha Wazo

Bomoa Pic Bomoabomoa yaja waliovamia kiwanda cha Wazo

Wed, 31 Aug 2022 Chanzo: Mwananchi

Bomoabomoa kubwa inakuja kwa waliovamia maeneo yanayomilikiwa na kiwanda cha saruji cha Wazo kilichopo katika Kata ya Wazo jijini hapa.

Hatua hiyo inafuatia kushindwa kwa wananchi hao kulipia maeneo waliyovamia na Serikali kutangaza kujitoa.

Wakazi hao ni wale wanaoishi maeneo ya Chasimba, Chatembo na Chachui katika Kata ya Wazo jijini humo.

Licha ya Serikali kuwawekea dhamana wananchi hao wapatao 4,070 ili wayanunue maeneo hayo ndani ya miezi sita, ni wananchi 39 tu sawa na asilimia tisa tu ndio wamelipia hadi sasa.

Akizungumza leo Jumatano Agosti 2022, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla baada ya kupokea taarifa ya kufanyika kwa kazi hiyo kutoka kwa uongozi wa kiwanda.

Amesema anawapa wananchi hao mwezi mmoja kukamilisha malipo hayo.

Advertisement "Katika kulitekeleza hilo watapita watu nyumba kwa nyumba kutoa ankara ya malipo na muhusika utatakiwa kusaini na kama hautaki ndio tutajua kuanzia hapo," amesema Mkuu huyo wa mkoa.

Makalla amesema baada ya hapo Novemba 1, 2022 watawakabidhi kiwanda eneo lao kwa ajili ya utekelezaji wa hukumu waliyoshinda kuwa wamiliki halali wa eneo hilo kufanya wanavyoona.

"Serikali tuliamua kutumia busara na huruma ili wananchi msiondolewe lakini mmeshindwa, tutakachokifanya ni kukabidhi majina tisa ya waliolipa na tutawapatia hati hao wengine watafute pakwenda," amesema Makalla.

Pia, ameonya suala hilo kuingiliwa na siasa na kueleza kuwa kuna watu wamekuwa wakipita kuwahadaa wananchi kuwa wasilipe na hakuna atakayewaondoa jambo ambalo halikubaliki kukaa kwenye hati ya mtu mwingine.

Kwa upande wao wananchi akiwemo, Fatma Saleh ameomba waongezewe muda kwani hata ambao hawajilipa sio kwamba wamependa bali ni kutokana na kuwa na vipato vidogo.

Stephano Kisimbo amesema uzito wa kulip umetokana na mkanganyiko ambapo awali waliambiwa wangelipa Sh1,000 hadi 2,000 kwa mita za mraba lakini ilipokuja kibadilishwa na kiwa Sh6,419 kwa mita za mraba ndio maana wakashindwa wengi kulipa.

Chanzo: Mwananchi