Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bomoa-bomoa Arusha Familia zalala nje

Bomoa Bomoa Rombo Bomoa-bomoa Arusha Familia zalala nje

Mon, 15 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Familia za watu saba zilizokuwa zikiishi katika nyumba za kupanga mtaa wa Mbeshere, jijini Arusha wamelazimika kulala nje kutokana na nyumba hizo kubomolewa kwa madai ya amri kutoka juu.

Mmiliki wa nyumba hizo aliyejimbulisha kwa jina la Frida Nicolaus amesema hakuwa na kesi yoyote na mtu, hivyo ameshangaa kubomolewa kwa nyumba zake ambazo moja ameijenge mwenye, nyingine za urithi, hivyo ameiomba serikali kuingilia kati sakata hilo.

Lawama Kubwa wamezielekeza kwa Dalali wa Mahakama anayefahamika kwa Jina Elibariki Mungure maarufu MOJAA, Wakidai hakuwa na nyaraka zinazomwelekeza kubomoa nyumba hizo.

Hata Dalali huyo amekanusha taarifa hizo kwa kueleza kuwa Mshinda tuzo aliyepewa haki na mahakama walifika ane eneo la tukio, kisha kupima eneo la hekari mbili, ambalo ndilo aliloeekezwa na mahakama kumkabidhi mteja wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live