Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodi yavunjwa kwa kushindwa kupambana na wizi pembejeo

0e055d5949f90b8080c1d35b8b7e7648 Bodi yavunjwa kwa kushindwa kupambana na wizi pembejeo

Fri, 18 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

BODI ya Chama Kikuu cha Ushirika cha Milambo LTD mkoani Tabora imevunjwa kwa kushindwa kushughulikia kikamilifu suala la wizi wa pembejeo zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 55 huku ikiamuriwa kuzirejesha pembejeo hizo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari ilisema, Mrajisi wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dk. Benson Ndiege alivunja bodi hiyo juzi kwenye kikao kilichofanyika mjini Urambo ambacho kilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Urambo, Angelina Kwingwa.

Ndiege baada ya kuvunja bodi hiyo aliwataka wajumbe wake kutoa ushirikiano kwa vyombo vya usalama ili waliosababisha au kuhusika katika wizi huo wa pembejeo wajulikane na kuchukuliwa hatua.

Vile vile alizuia wajumbe wa Bodi iliyovunjwa kutogombea uongozi wa bodi katika Vyama vyao vya Ushirika vya Msingi na Chama Kikuu.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya hiyo Angelina Kwingwa alisema kuwa baada ya kupewa taarifa ya wizi wa pembejeo uliotokea katika Chama Kikuu cha Ushirika cha Milambo alikwenda na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama kwenye Ghala la chama hicho ulipotokea wizi na kufanya mahojiano na Wahusika.

Chanzo: habarileo.co.tz