Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodi ya wadhamini TaFF yakagua kiwanda cha mazao ya nyuki

9449dbd93012a8934088a45a1f97a996 Bodi ya wadhamini TaFF yakagua kiwanda cha mazao ya nyuki

Wed, 31 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF) imekagua mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kuchakata na kufungasha mazao ya nyuki uliopatiwa ruzuku na mfuko huo unaotekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe mkoani Geita.

Mfuko wa Misitu Tanzania unagharamia asilimia 95%, huku Halmashauri ya Wilaya Bukombe ikichangia asilimia tano za ujenzi wa kiwanda hicho kitakachoendeshwa na Halmashauri ya Bukombe kwa mfumo wa Kampuni Tanzu (SPC).

Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini (TaFF), Profesa Romanus Ishengoma amesifu ujenzi unaoendelea na kuitaka halmashauri hiyo kushirikiana kwa karibu zaidi na bodi hiyo.

“Utajiuliza je asali ipo tunaweza kuweka hapa kiwanda cha milioni 500, fedha ya serikali tumeitumia. Uamuzi ni wa kwetu kama bodi sasa kitakamilika ukajikuta unazunguka asali ipo wapi?” aliohoji Prof Ishengoma.

Katibu Tawala wa Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF), Dk Tuli Msuya amesema ni vema mchakato wa kuanzisha kampuni tanzu uanze sasa kama lilivyosaini kwenye mkataba wa ujenzi wa kiwanda hicho.

“Suala la kampuni Tanzu siyo hiari kwa sababu tulisaini mkataba tukakubaliana kwamba tutaanzisha kampuni tanzu ya kusimamia hichi kiwanda, ni vema tukaanza mchakato tukapokamilisha ujenzi wa kiwanda kampuni inakuwa tayari ipo na inaanza kufanya kazi”alisema Msuya.

Kamishna Mhifadhi Mkuu wa Misitu (TFS), Prof Dos Santos Silayo amesema wilaya hiyo inasifika kwa kuzalisha asali nzuri na taarifa zinaonyesha kuwa asali nyingi inayozalishwa wilayani humo inapelekwa nje na wafanyabiashara, si jambo baya kwa sababu ni mmonyororo mzima wa biashara.

“Tujipange kupambana kibiashara, tunatakiwa kuangali mazingira ya kibiashara ya kuifanya asali isiende nje ikiwa ghafi bila ya kupita katika kiwanda hiki, hatuwezi kusema asali ya Tanzania isiuzwe nje, lakini tunapambana nayo kibiashara,”alisema Silayo.

“Tutakaponunua vifaa kwa ajili ya kiwanda tuangalie vile ambavyo vitakuwa na uwezo wa kuchakata mazao mbalimbali ya asali, tunakiwa kuwa makini na kutazama mbali,” aliongeza Silayo.

Mapema Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Said Nkumba amesema kutokana na maeneo hayo kuzungukwa na hifadhi kumekuwa na mazingira bora na salama ya kufuga nyuki wanaozalisha asali bora kwa sababu ya kutokuwa na mwingiliano na shughuli za binadamu.

“Ujio wa kiwanda hiki umekuja sehemu sahihi kwa sababu kitakuwa kiwanda endelevu kwa kuwa wakazi hapa ni wafugaji nyuki hivyo kurahisisha upatikanaji wa malighafi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Temeke na Mjumbe wa Bodi TaFF, Godwin Gondwe amesema angependa mkurungezi wa halmashauri ajue hiki ni kiwanda cha Serikali kwa lengo la kuongeza mapato ya wilaya.

“Ukiangalia jinsi ya uchangiaji wa fedha za ujenzi utaona Halmashauri imetoa asilimia ndogo ya kile wanachotakiwa kuchangia wakati Bodi imetoa zaidi ya asilimia 50 ya fedha zote kwa hiyo commitment yao haionekani,” amesema Gondwe.

Chanzo: www.habarileo.co.tz