Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodaboda waonywa kupakia mshikaki Manyara

Bbb Bodaboda waonywa kupakia mshikaki Manyara

Fri, 4 Nov 2022 Chanzo: Eatv

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Manyara, Mrakibu Msaidizi  SP. Georgina Matagi, ametoa wito kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri waliopigwa faini kulipa kabla hawajachukuliwa hatua.

Kamanda Matagi amewaonya madereva bodaboda wenye tabia za kupakia abiria kuacha kuwakimbia askari wa usalama barabarani wanapo wasimamisha kwani kwa kufanya hivyo ni kuhatarisha usalama wao pamoja na Abiria.

Kamanda Matagi amefikia uamuzi huo kufuatia wengi wa wamiliki wa vyombo vya usafiri kutolipa madeni hayo huku ajali zikidaiwa kutokea kwa dereva boda wanaokimbia askari wa barabarani.

Kuhusu dereva bodaboda kupakia watu mshikaki na kuhatarisha maisha ya abiria haswa wanaposimamishwa na kukimbia Kamanda Matagi anasema, huku Afisa Usalama Barabarani Kiteto akitahadharisha boda kwa vitendo vya kutekwa.

Nao baadhi ya madereva hao wakizungumza na Kiongozi huyo wa Usalama Barabarani Mkoa wa Manyara wameeleza changamoto zao zikiwemo faini zisizo na utaratibu.

Chanzo: Eatv