Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodaboda avunjika taya baada ya kugonga gari

54651 Pic+taya

Tue, 30 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Haraka haraka haina baraka, ndivyo unavyoweza kusema kwa tukio la mwendesha bodaboda, Wambura Getuti (25) mkazi wa Chamoto, Mugumu wilayani Serengeti ambaye amevunjika taya baada ya kugonga gari lililoegeshwa.

Boda huyo ambaye anaaminika kwa mwendo wa ‘kujitungua’ alikumbwa na mkasa huo Aprili 28,2019 saa 8 mchana katika eneo la Posta ya zamani.

John Getuti, kaka wa Wambura akizungumza na Mwananchi Digital katika Hospitali Teule ya Nyerere leo Jumatatu, Aprili 29,2019, amesema mdogo wake huyo ambaye hawezi kuzungumza aliliingia kwa nyuma gari aina ya Toyota wakati akikwepa bajaji iliyoingia ghafla barabarani.

Amesema baada ya kuanguka walimchukua hadi hospitali na baada ya vipimo walibaini taya limevunjika,  akilalamika maumivu kifuani na wanaendelea na uchunguzi zaidi.

Hata hivyo baadhi ya mashuhuda wanadai alikuwa mwendo kasi maarufu kama ‘kujitungua’ na akawa anatoa simu mfukoni ili azungumze nayo huku mbele yake kukiwa na bajaji, na wakati anaikwepa akiwa kasi akaingia nyuma ya gari lililokuwa limeegeshwa.

Mganga wa zamu katika hospitali hiyo, John Nyang'ombe amesema wanasubiri ripoti ya wataalamu wa meno kujua kama itabainika hawawezi kushona taya, watampa rufaa kwenda Hospitali ya Rufaa ya Bugando Mwanza kwa ajili ya matibabu zaidi.

Related Content



Chanzo: mwananchi.co.tz