Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodaboda auwawa kwa kupigwa risasi Geita

Gun Shooting 1 Bodaboda auwawa kwa kupigwa risasi Geita

Wed, 2 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kijana Mmoja anayefahamika kwa Jina Amini Salum Mkazi wa Mtaa wa Nyamarembo Wilaya ya Geita Mkoani Geita, amepigwa risasi na Majambazi usiku wa kuamkia juzi wakati akifanya shughuli zake za Bodaboda majira ya usiku.

Wakizungumza baadhi ya Rafiki zake ambao amekuwa akifanya nao kazi za Bodaboda akiwemo mmoja wa Vijana aliyekuwa amepakiwa usiku huo wakati tukio linatokea, amesema wakati tukio hilo linatokea Majambazi hao walikuwa na gari ambalo hawakuweza kulifahamu ambapo baada ya kumuona Bodaboda huyo alimiminiwa risasi na kufariki dunia.

“Ilikuwa leo kama Mida ya saa kumi na moja na dakika arobaini na tano hivi nilikuwa kijiweni kwangu hapa ikaja gari ya polisi ambayo alikuwemo askari mmoja ni Jamaa yetu mmoja amepanga hapo juu alipofika akageuza hapo gari akapaki akaniuliza tukasalimiana naye pale akanihoji Amini huwa anakaa wapi nikamwelezea, swali la pili akaniuliza je Amini huwa anakaa na wazazi wake au anafamilia nikamwambia anafamilia alichoniambia aliniambia hatuko naye Duniani, ‘ Bodaboda.

Sofia Jongo ni Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita amekiri kuwepo kwa tukio hilo la mauaji lililofanywa na Majambazi huku lengo lao likiwa ni kupora Mfanyabiashara huyo ambaye Jina lake limehifadhiwa na Jitihada za kuwatafuta Majambazi hao zikiendelea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live