Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodaboda, Machinga Arusha kumuaga JPM Dodoma

58b06e841c1b508a12e903c4e49fafa2 Bodaboda, Machinga Arusha kumuaga JPM Dodoma

Mon, 22 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Viongozi wa waendesha bodaboda Mkoa wa Arusha, wafanyabiashara wadogo na wanachama wao wanatarajia kwenda Dodoma kumuaga aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli.

Waliyasema hayo jana baada ya kusaini kitabu cha maombolezo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha. Walisema lazima waende Dodoma kumuagfa Magufuli kwa kuwa aliwathamini na alikuwa mtetezi wao.

Mwenyekiti wa waendesha Boda Boda Mkoa wa Arusha, Godlite Rugemalila alisema kifo cha Magufuli ni pigo kwa bodaboda mkoa Arusha na Tanzania kwa ujumla.

Rugemalila alisema Magufuli aliwapenda bodaboda na kuwapa uhuru wa kufanya biashara bila bugudha na hilo lilikuwa faraja kubwa kwao hivyo lazima waende Dodoma kumuaga.

Mwenyekiti wa wafanyabiashara ndogondogo maarufu kwa jina la Machinga, Amina Chonga alisema vilio vilitawala katika soko kuu Arusha, soko la Kilombero, kwenye uuzwaji wa nguo za mitumba eneo la Krokoni, na barabarani baada ya taarifa za kifo cha Magufuli.

Aliwataka Machinga mkoani Arusha wawe na moyo wa subira na wasiendelee kusononeka.

Alisema, Magufuli alikuwa kiongozi aliyekuwa akijali maendeleo ya Watanzania hasa wanyonge na alikuwa mstari wa mbele kukemea waliotaka kujinufaisha.

Mfanyabiashara jijini Arusha, Richard Paul alisema kifo cha Magufuli ni pigo kubwa kwa nchi na akaomba Rais Samia Suluhu Hassan amuenzi kwa kuendeleza miradi yote mikubwa kwa faida ya Watanzania.

Paul alisema Magufuli alitaka nchi ijitegemee kiuchumi hivyo viongozi waliobaki wahakikishe miradi yote mikubwa aliyoiacha Magufuli inatekelezwa.

Chanzo: www.habarileo.co.tz