Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Biteko: Vijiji vyote Iringa vina umeme

Mgao Umeme.jpeg Biteko: Vijiji vyote Iringa vina umeme

Fri, 23 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

erikali imesema usambazaji umeme Vijijini Mkoani Iringa umefanyika kwa asilimia 100 ambapo Vijini vyote 360 Mkoani humo vimesambaziwa umeme kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amesema hayo akiwa Mkoani Iringa kwa ajili kuwasha umeme na kukagua miundombinu ya umeme ambapo amesema usambazaji umeme katika Vjtongoji vya Mkoa huo umetekelezwa kwa asilimia 64.11 na Vitongji 1,188 vimesambaziwa umeme kati ya 1,853.

Baada ya kuwasha umeme kwenye Kijiji cha Mkangwe Wilayani Mufindi, Dkt. Biteko amewataka Wakandarasi wa miradi ya usambazaji umeme Vijijini kutekeleza kazi kwa wakati ili kuendana na kasi ya maendeleo huku akiiagiza REA kuwachukulia hatua Wakandarasi wazembe.

Amewapongeza Wakandarasi wa umeme Vijijjni waliofanya kazi ya usambazaji Mkoani Iringa ambayo imepelekea Vijiji vyote Mkoani humo kuwa na umeme hadi kufikia December 2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live