Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Biteko: Tanesco, Tarura fikisheni huduma Ngorongoro

Mkandarasi JNHPP Amelipwa Kwa Zaidi Ya Asilimia 80   Biteko Biteko: Tanesco, Tarura fikisheni huduma Ngorongoro

Tue, 16 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko ameagiza Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kuhakikisha linapeleka huduma ya umeme kwenye maeneo ya miradi ya maendeleo ili kuharahisisha huduma kwa wananchi.

Dk. Biteko amesema hayo akiwa Loliondo, wilayani Ngorongoro baada ya kuzindua minara ya kurushia matangazo ya TBC Taifa na Bongo fm.

Amesema miradi inatekelezwa na itakuwa ya mafankio endapo Taasisi husika zitakaa pamoja na kuandaa maeneo yanayohitaji utekelezaji katika hatua mbalimbali.

"TANESCO, REA, UCSAF na TBC zikae pamoja wakati wa uandaaji wa miradi husika ili miradi iwe inatekelezeka kwa tija, ufanisi na kwa haraka".

Pia, ameiagiza TARURA kuhakikisha huduma ya barabara zinafikika katika maeneo ilipojengwa mitambo ya redio ambayo ipo sehemu kubwa ya milimani nchini ili kuwa na miundombinu imara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live