Binti anayefahamika kwa jina moja la Leah (19) mkazi wa manispaa ya Bukoba mkoani Kagera amepoteza maisha baada ya kusombwa na maji, huku baadhi ya barabara zikifungwa kutokana na mvua kubwa za mafuriko zinazoendelea kunyesha.
Binti anayefahamika kwa jina moja la Leah (19) mkazi wa manispaa ya Bukoba mkoani Kagera amepoteza maisha baada ya kusombwa na maji, huku baadhi ya barabara zikifungwa kutokana na mvua kubwa za mafuriko zinazoendelea kunyesha. Kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Kagera SACF Zabron Muhumha amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataka wananchi hasa wa manispaa ya Bukoba kuchukua tahadhari barabarani na kwa wale wanaoishi kwenye maeneo ya bondeni kuhama.