Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Binti auawa, mwili wakutwa chumbani kwa wazazi wake

Maiti Mauaji Kifo 58 Instagram Binti auawa, mwili wakutwa chumbani kwa wazazi wake

Thu, 14 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwili wa binti Vanesa Bukuku miaka 18 mkazi wa Mtaa wa kaani Mjini Tunduma mkoani Songwe umekutwa uvunguni Mwa kitanda chumbani kwa wazazi wake ukiwa na Majeraha shingoni.

Akizungumza Mama mzazi wa Marehemu anadai kuwa baada ya kurudi nyumbani juzi Machi 12, 2024 Majira ya saa moja jioni alipata taarifa ya kuwa binti yake hakuonekana tangu saa saba mchana hivyo katika jitihada za kumtafuta aliona tone la Damu sebleni kwake lililoelekea chumbani lililomshawishi kufuatilia mpaka uvunguni mwa kitanda chake.

Mama anadai kuwa baada ya kuangalia aliona mwili wa Mtoto wake uliokuwa umetapakaa damu akaanza kupiga kelele kuita majirani ambapo baada ya kuangalia waligundua ni Mwili wa binti huyo.

Jana Machi 13, 2024 Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Songwe Kamishina Msaidizi Mwandamizi SACAP Theopista Malya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea siku ya juzi Machi 12, 2024 majira ya saa 1 jioni.

Kamanda Malya amedai kuwa jeshi la polisi linamshikilia mtu mmoja kwa mahojiano na taratibu zingine za uchunguzi zinaendelea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live