Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Binti auawa, atupwa nyuma ya ofisi

Binti Picds Binti auawa, atupwa nyuma ya ofisi

Fri, 18 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kifo cha Anna Haule (26), mkazi wa Mtaa wa King’ongo, jijini hapa kimeacha maswali baada ya mwili wake kukutwa nyuma ya ofisi za Serikali ya Mtaa wa Michungwani, Kata ya Saranga.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Mtafilo Kipingu hakupatikana jana kutoa ufafanuzi wa tukio hilo, licha ya simu yake kuita bila kupokewa.

Tukio hilo lililotokea usiku wa kuamkia Julai 29 liliibua taharuki, baada ya maelfu ya wakazi kufurika nyuma ya ofisi hizo kushuhudia mwili wa binti huyo aliyekuwa mtoto wa pili kati ya watatu wa familia ya Yusinta Lupembe.

Inadaiwa kuwa binti huyo aliondoka nyumbani saa 11 jioni Julai 28 na mwili wake kuonekana saa 3:00 asubuhi.

“Alipomaliza kupika akaondoka jioni saa 11 jioni, akaenda kituoni hapo mwishoni King’ongo,” alisema mama wa binti huyo huku kaka yake, Edimund akidai saa 4:00 usiku alimpigia simu akitaka aende kwake lakini alimkatalia.

“Mie nilimkatalia nikamwambia (Anna) usiku huu pumzika nyumbani.”

Mwenyekiti wa Mtaa wa Michungwani, William Chitanda alidai binti huyo huenda ameuawa na vijana wa mtaa mwingine kisha kutupwa mtaani kwake.

“Tuna vijana 60 wa ulinzi shirikishi ambao wanaimarisha ulinzi kwa zone (kanda) nane, nakuhakikishia wahalifu wametoka naye Mtaa wa King’ongo.”

Mwenyekiti wa Mtaa wa King’ongo, Tatu Pambe alisema taarifa za uchunguzi wa awali, Anna aliuawa na vijana waliomchukua usiku katika maeneo ya starehe. “Alionekana usiku huo (Julai 29) katika kibanda cha pombe kali, baadaye akaondoka na vijana wawili kwa bodaboda kuhamia Nyura Pub,” alisema Pambe.

Adam, muuzaji wa pombe kali eneo hilo la King’ongo alikiri kumpokea Anna usiku saa 4:00 kabla ya kuelekea katika Pub ya Kimara King’ongo ambako alitoka saa 5:00 usiku kama ilivyothibitishwa na mhudumu aliyekuwa zamu usiku huo, Ester Daud.

Baada ya kutoka pub hiyo alichukua bodaboda akiwa na vijana hao wawili, lakini haikufahamika bodaboda aliyewachukua kama ilivyothibitishwa na dereva wa bodaboda kituo cha King’ongo, Silverio Simon.

“Hapa hakuna anayepaki hadi saa sita usiku, inawezekana alichukua bodaboda wa njiani,” alisema.

Katika ufuatiliaji wa tukio, gazeti hili lilifika katika baa ya mwisho aliyokunywa pombe, ambayo ilifungwa saa saba usiku kama ilivyothibitishwa na muhudumu aliyekuwa zamu usiku huo, Doto Kitomari. “Kuna vijana wengi hapa, sasa siwezi kujua aliondoka na nani, mie nilikuwa kaunta.”

Pub hiyo inapatikana Mtaa wa Michungwani, mita 100 kutoka eneo ambalo mwili wa Anna ulikutwa saa 3:00 asubuhi ukiwa chali na miguu ya njano, ikiwa pia ni nyuma ya Pub hiyo.

Hata hivyo, uchunguzi wa gazeti hili haukuthibitisha wala kutambua vijana waliodaiwa kuhusika kama ni wakazi wa eneo hilo au wanatoka mitaa mingine.

Kaka wa Anna, ambaye ni Edmumnd alisema wanatarajia kufanya maziko kesho Jumatatu baada ya kukamilika hatua zote za uchunguzi wa mwili wake uliohifadhiwa katika Hospitali ya Mlonganzila.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live