Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Binti atuhumiwa kwa uchawi, akutwa na mchanga

Binti Hatariii Binti atuhumiwa kwa uchawi, akutwa na mchanga

Wed, 26 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Flora Juma (18), ambaye amekuwa akifanya kazi za ndani katika familia moja iliyopo mtaa wa Kombo Masai, Kata ya Malolo Mjini Tabora, amejikuta yuko matatani kwa kutuhumiwa na uchawi, baada ya bosi wake kukagua na kukuta begi lake lina dawa za kienyeji.

Mama wa familia ambayo binti huyo amekuwa akifanya kazi za ndani  Shamira Ngoma, amesema alianza kupata sintofahamu juu ya binti huyo baada ya siku ya kwanza kumkagua  katika begi lake alipofika na kukuta kifurushi cha dawa za kienyeji ambapo binti huyo alimweleza hutumia dawa hizo katika kujitibu maumivu ya tumbo ambayo husumbuka nayo.

Aidha Shamira, amesema mwenendo wa maisha ya binti nyumbani hapo uliendelea kumchanganya, kwani wakati mwingine alikuwa akifanya vitu kama mtu asiyekuwa na utimamu wa akili, hatua iliyomfanya kufikia uamuzi wa kutaka kumrudisha nyumbani kwao wilayani Kahama mkoani Shinyanga ambapo wakati akimwandalia nguo katika begi lake tayari kwa kumsafirisha alikuta tena mchanga na shanga vikiwa vimefungashwa kwenye karatasi.

Kwa upande wake Flora akijibu tuhuma ya ushirikina dhidi yake amesema mchanga na shanga vilivyokutwa ndani  ya begi lake aliagizwa na bibi yake ambaye alimtokea kimazingara usiku wa Oktoba 23 mwaka huu, wakati akiangalia runinga sebuleni na kumwambia achote mchanga nje ya nyumba ya familia hiyo na badae ataufata bila yeye kujua utakwenda kufanyiwa kazi gani .

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo wa Komba Masai, Dotto Kitungulu, amefika katika nyumba ya familia hiyo ambapo amehakikisha usalama wa binti huyo ambaye alikuwa amezingirwa na  wananchi mpaka aliposafirishwa  kurudi nyumbani kwao mkoani Shinyanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live