Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Binti anamtafuta baba yake aliyepotea Dar

72589 Amepotezapic

Thu, 22 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mzee anayefahamika kwa jina la Hassan Abdallah Kitele (76) mkazi wa Tandika jijini Dar es Salaam anadaiwa kutoweka nyumbani kwake tangu siku saba zilizopita.

Akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi Agosti 22, 2019 mtoto wa mzee Kitele, Fatuma Kitele amesema  baba yake aliondoka nyumbani kwao bila kuaga Agosti 15,2019 asubuhi.

Fatuma amesema walipobaini baba yao hajarudi nyumbani kwa siku ya kwanza walianza kumtafuta bila mafanikio.

Ameeleza kuwa baadaye walitoa taarifa katika kituo cha polisi cha  Chang’ombe jijini Dar es Salaam.

“Wakati anaondoka alivaa shati na suruali vyenye rangi ya kijivu, kofia ya blue na pia amekuwa akipoteza kumbukumbu mara kwa mara,” amesema Fatuma.

Mwanae huyo wa kike amesema tayari wameshafika kwenye vituo vya polisi mbalimbali, hospitali na shambani kwake Mkuranga mkoani Pwani alikokuwa anapaenda kutembelea huko kote hawajafanikiwa kumuona.

Pia Soma

“Mtu yeyote akimuona baba yetu tunaomba atupigie simu kwa namba 0782641191  au namba ya polisi ambayo ni  0759015351,” amesema Fatuma.

Chanzo: mwananchi.co.tz