Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Binti afariki kwa kupigwa na radi

Radi Binti afariki kwa kupigwa na radi

Wed, 21 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Calista Haulep (15) mkazi wa kijiji cha Lifua kata ya Luilo wilayani Ludewa mkoani Njombe amefariki baada ya kupigwa na radi wakati akiwafunga mbuzi chini ya mti baada ya kuwatoa malishoni.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamesema binti huyo alipigwa na radi hiyo na kufa papo hapo sambamba na mbuzi aliokuwa akiwafunga.

Baba wa binti huyo pamoja na dada yake wameelezea masikitiko yao na kudai kuwa binti huyo alirejea nyumbani wiki moja iliyopita akitokea shuleni Mafinga mkoani Iringa kwa ajili ya likizo baada ya shule kufungwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live