Serikali kupitia Mradi wa kuboresha Miundombinu katika Jiji la Dar es Salaam (DMDP) imetenga Sh bilioni 8.4 kwa ajili ya ujenzi wa mfereji wa maji ya mvua wenye urefu wa kilomita 8.89 katika Kata ya Mbweni.
Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Felista Njau aliyehoji Serikali ina mkakati gani wa kutatua tatizo la mafuriko katika maeneo ya Mbweni Teta, Bunju Basihaya, Kunduchi, Nyamachabes, Ununio na Mikocheni katika Jimbo la kawe.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi Ya Rais -TAMISEMI, Naibu Waziri wa Wizara hiyo, David Silinde alisema kuwa Serikali inambua changamoto ya mafuriko katika maeneo ya Mbweni Teta, Bunju Basihaya, Kunduchi, Nyamachabes, Ununio na Mikocheni katika Jimbo la kawe.
Serikali itaendelea kujenga na kukarabati miundombinu ya barabara, madaraja na mifereji ya maji ya mvua ili kuondoa kero ya mafuriko katika meneo mbalimbali Jijini Dar es Salaam ikiwemo Jimbo la Kawe.
“Awamu ya pili ya mradi huu itajumuisha Mifereji ya Maji ya Mvua katika maeneo ya Kunduchi, Nyamachabes, Ununio na Mikocheni,” alisema Silinde.