Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bilioni 8.2 kutumika ujenzi gereza jipya Geita

Gereza Gerezaaaaaaaaaaaa (600 X 360) bilioni 8.2 kutumika ujenzi gereza jipya Geita

Mon, 22 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

JESHI la Magereza nchini linatekeleza miradi sita ya ujenzi wa magereza mapya nchini likiwemo la Wilaya ya Gairo ,mkoani Morogoro ambalo litagharimu kiasi cha Sh bilioni 8.2 hadi kukamilika kwake.

Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, Ramadhan Nyamka amesema hayo katika taarifa yake kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla wakati wa halfa ya uwekaji jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa gereza la wilayani Gairo katika shamra shamra za kuadhimisha miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Nyamka amesema ujenzi wa gereza hilo ulianza rasmi Julai 15, 2023 kwa njia ya Force Akaunti na utekelezaji wake umepangwa kufanywa kwa awamu nne, na lengo ni kusogeza huduma ya magereza karibu na wananchi wa mji wa Gairo.

Amesema mradi wa ujenzi wa gereza hilo unajumuisha ujenzi wa jengo la utawala , mabweni matano ya kulaza wafungwa , ghala la kuhifadhi chakula, bwalo , nyumba za watumishi na uzio.

Nyamka amesema gereza hilo litakuwa na uwezo wa kuhifadhi wafungwa 500 kati ya hao wanaume 450 na wanawake ni 50 na litakuwa ni sehemu ya kupunguza msongamano katika magereza ya jirani pia kupunguza adha ya kuwasafirisha umbali mrefu wahalifu kwa ajili ya huduma za kimahakama.

Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo amesema kwa kuanzia Mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali iliidhinisha jumla ya Sh milioni 767.2 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la utawala na mabweni mawili ya wafungwa wakiume na ghala la silaha.

Amesema hadi kufikia Aprili Mwaka huu (2024) jumla ya Sh milioni 378.6 zilipokelewa na kutumika kukamilisha ujenzi wa jengo la utawala na bweni moja la wanaume.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live