Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bilioni 73/- kukarabati uwanja wa ndege Songea

RUNWAY Bilioni 73/- kukarabati uwanja wa ndege Songea

Mon, 20 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

SERIKALI imetoa shilingi bilioni 73 kukarabati na kupanua uwanja wa ndege Songea mkoa wa Ruvuma ili kupanua na kukuza wigo wa mawasiliano ya usafi ri wa anga mkoani humo.

Mkuu wa Mkoa huo, Christina Mndeme amesema hayo jana wakati akizungumza na Habarileo ofisini kwake mjini Songea. Alisema uwanja huo unatarajiwa kufunguliwa Agosti mwaka huu na kwamba, kwa sasa ujenzi wake umekamilika kwa asilimia zaidi ya 90.

Kwa mujibu wa Mndeme, utakapokamilika ndege kubwa ikiwemo Bombadier zinataanza kutua. Mhandisi mshauri wa ujenzi huo, Jofrey Keneth amesema wamefikia hatua nzuri sasa.

“Hivi sasa ndege ndogo zinatua kwenye uwanja mpya ambao umefunguliwa, uwanja umejengwa kwa mita 800 na mkandarasi ataongeza mita nyingine 400 kupata mita 1200 ndege kubwa ziweze kutua na kuruka,’’ alisema Keneth.

Alisema hadi mwishoni mwa Agosti mwaka huu atakuwa amekamilisha kujenga uwanja kwa mita 1,200 ambazo ndizo hitaji la chini zaidi kuwezesha kutua ndege aina ya Bombardier. Meneja wa TANROADS Mkoa wa Ruvuma Lasack Alinanuswe alisema Serikali imetoa shilingi bilioni 39 kutekeleza mradi huo. Alisema mradi huo tangu uanze, kampuni ya CHICCO kutoka China imeajiri wafanyakazi 110 Watanzania wa Ruvuma na Wachina saba.

“Mhandisi wa ujenzi huo hivi sasa anafanya kazi usiku na mchana ili aweze kukamilisha kazi hiyo ndani ya mkataba, Juni 28 mwaka huu tulihamisha shughuli za urukaji wa ndege kutoka upande wa zamani wa 14 kwenda upande mpya wa 32 kwa hiyo hivi sasa ndege zinatumia uwanja mpya,’’ alisema Alinanuswe.

Chanzo: habarileo.co.tz