Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bilioni 5.7 zatolewa kutatua changamoto ya miundombinu Songwe

Songweeeeeeee Bilioni 5.7 zatolewa kutatua changamoto ya miundombinu Songwe

Mon, 6 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Daniel Chongolo ameipongeza timu ya wataalamu wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) kwa kufanya kazi kwa haraka na ufanisi mkubwa kuhakikisha barabara zinapitika mkoani Songwe.

Rc Chongolo ameeleza kuwa changamoto ya uharibifu mkubwa wa miundombinu umefanyiwa kazi kwa haraka na timu ya wataalamu wa TANROADS na TARURA jambo ambalo limerejesha mawasiliano ya pande zote zilizokuwa hazipitiki.

"Kila mmoja kwa barabara zake wamefanya kazi kubwa na wanaendelea kufanya hivyo lengo ni kuhakikisha Wananchi hawakosi huduma ya barabara pale inapotokea changamoto’’ Amekaririwa Mhe Chongolo

Kwa upande wake Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Songwe Mhandisi Suleiman Bishanga akizungumza mara baada ya kukagua sehemu zilizoathirika na mvua za El-Nino wilayani Songwe na Ileje amesema kuwa Serikali inayoongozwa na Rais Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa zaidi ya shilingi Bilioni 5.7 kwa ajili ya kutatua changamoto na kurejesha miundombinu ya barabara na madaraja ambayo yameharibiwa na mvua kubwa za El- nino zinazoendelea kunyesha Mkoani Songwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live