Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bilioni 44/- zapitishwa bajeti ya Misungwi

3bebf0c134128365ef8db64e2441db43 Bilioni 44/- zapitishwa bajeti ya Misungwi

Fri, 19 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

HALMASHAURI ya Wilaya ya Misungwi imepitisha bajeti ya Sh bilioni 44 kwa ajili ya mwaka wa fedha 2020/2021.

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Kashinje Erasto katika kikao cha bajeti hiyo.

‘’Bajeti ni kubwa na tutatekeleza miradi mbalimbali. Wajibu wetu kama madiwani, ni kuhakikisha tunakuwa wasimamizi wazuri na kuiona hii miradi ni ya kwetu,” alisema Erasto.

Aliwataka madiwani wenzake kuwa na utamaduni wa kuhakikisha wanashiriki vyema katika miradi.

‘’Tulikuwa na ombi la fedha kwa ajili ya ukamilishaji wa hospitali ya wilaya, serikali ilitenga Sh bilioni 1.3 na tayari zimetufikia kwa ajili ya ukamilishaji wa hospitali hiyo,” alisema Erasto.

Kuhusu maombi ya ukamilishaji wa jengo la utawala la halmashauri, alisema wamepokea Sh milioni 600 na ukarabati wa jengo hilo unaendelea ukitarajiwa kukamilika ndani ya miezi miwili ijayo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Kisena Mabuba, alisema madiwani wamesisitiza uibuaji wa vyanzo vipya vya mapato.

“Moja ya vyanzo vipya vya mapato tumeamua kuweka fidia kwa maeneo ya Nyashishi na tunatarajia kujenga stendi ya daladala pamoja na soko la mbogamboga,” alisema Mabuba.

Alisema katika eneo la Nyashishi, wamelipa fidia ya Sh milioni 216 na hadi sasa inadaiwa Sh milioni 26. Fedha hizo zitalipwa mwaka katika ujao wa fedha.

Aidha, Mabuba alisema watalipa fidia pia kwa wananchi walio katika Kisiwa cha Buzumo. Halmashauri inalenga kugeuza eneo hilo ili liwe kivutio cha watalii.

Alisema watazungumzia na Wizara ya Maliasili na Utalii ili wapeleke wanyama wasiokuwa wakali katika kisiwa hicho.

Chanzo: habarileo.co.tz