Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa amesema Serikali imetenga shilingi Bilioni nne kwa ajili ya kuongeza mtandao wa barabara wilayani Mtama mkoani Lindi.
Waziri Mchengerwa ameyasema hayo alipokuwa akisalimia Wananchi wa Mtama waliokusanyika kumsikikiza Rais Samia Suluhu Hassan akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Lindi.
Ameongeza kuwa tayari Serikali imekwishatoa shilingi Bilioni moja za kwenda kujenga na kukarabati hospitali ya wilaya ya Mtama.
Aidha, Waziri Mchengerwa amesema Serikali kupitia Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imekwshaweka taa za barabarani 35 na katika bajeti mpya ya mwaka wa fedha wa 2023/2024 zimetengwa fedha kwa ajili ya kuongeza taa.