Thu, 30 Nov 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Wanafunzi wa kike 1,000 wanatarajia kunufaika na mradi wa shule ya sekondari ya wasichana Mkoa wa Simiyu inayojengwa katika eneo la Igegu wilayani Bariadi kwa thamani ya shilingi bilioni nne.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu, Shemsa Mohamed amesema ujenzi wa shule hiyo umefika asilimia 17 na kuagiza shule hiyo kukamilika ifikapo Januari 10, 2024.
Mohamed ameyasema hayo wakati wa ziara iliyofanywa na kamati ya siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live