Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bilioni 4.7 zilivyobadili sekta ya afya Kigoma

Bilioni 4.7 Zilivyobadili Sekta Ya Afya Kigoma Bilioni 4.7 zilivyobadili sekta ya afya Kigoma

Fri, 15 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluh Hassan imetoa Zaidi ya shilingi Bilioni 4.7 katika kuboresha huduma za afya halmashauri ya wilaya ya Kigoma na kuwezesha wananchi kuanza kupata huduma maeneo ya karibu.

Akizungumza ofisini kwake mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Bi. Rose Manumba amemshukuru Rais Samia kwa kuonyesha upendo kwa wananchi wa Kigoma ambapo kwa miaka mitatu sekta hiyo ya afya imebadilika kwa ukubwa wake.

Aidha amesema kuwa kiasi hicho cha fedha kimewezesha halmashauri hiyo kujenga vituo vitatu vya afya vipya, Hospitali ya wilaya sambamba na Zahanati ambapo wananchi kwasasa hawatembei umbali mrefu kuzifata huduma hizo tofauti na ilivyokuwa miaka mitatu nyuma.

Wakiongea kwa nyakati tofauti wananchi katika halmashauri hiyo wameipongeza serikali kwa kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu wa kufata huduma za afya ambapo wameelezea kuwa kwa kipindi cha nyuma wanawake wengi walikuwa wakijifungulia njiani wakipelekwa kwenye zahanati za mbali na maeneo yao

James Kayunguye ni mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Kigoma ambaye amesema kuwa sekta ya afya katika halmashauri ya wilaya ya Kigoma imeimarika Zaidi kwa kuongezeka kwa vituo vya afya na zahanati hasa katika mwambao wa ziwa Tanganyika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live