Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bilioni 36/- zatumika kununua vivuko, boti

5143a11bce607197ec54cbb85e390a09 Bilioni 36/- zatumika kununua vivuko, boti

Sat, 24 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WIZARA ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Tano, imetumia Sh bilioni 36.36 kwa ajili ununuzi wa vivuko na boti zinazotoa huduma ya dharura.

Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Elius Mwakalinga alisema hayo wakati wa uzinduzi na kukabidhi Kivuko cha MV Pangani 11 katika eneo la Feri wilayani Pangani juzi.

Alisema katika kipindi hicho, wizara hiyo kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa) pia imefanikiwa kufanya ukarabati mkubwa wa vivuko sita vinavyotumika katika maeneo mbalimbali nchini.

Alisema vivuko hivyo vinarahisisha usafiri wa abiria na mizigo na wananchi wanakuwa na uhakika wa usalama wao na mali zao na kusaidia ukuaji wa uchumi kwenye maeneo hayo.

"Kwa kuwa vivuko ni rasilimali muhimu ya taifa na vinahitajika na wananchi wengi hususani hapa Pangani, hivyo nawaomba Temesa kusimamia ukarabati vivuko ili viweze kufanya kazi iliyokusudiwa," alisema.

Mtendaji Mkuu wa Temesa, Japhet Masele alisema Kivuko cha MV Pangani 11, ukarabati wake umegharimu Sh milioni 497.01.

"Kivuko hiki baada ya ukarabati mkubwa kina uwezo wa kubeba tani 50 kwa maana ya magari madogo manne pamoja na abiria 100 kwa wakati mmoja," alisema.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela aliiomba wizara hiyo kukamilisha kwa wakati mchakato wa fidia kwa wananchi waliopo kwenye barabara ya Tanga hadi Pangani, ambao ujenzi wake kwa sasa upo kwenye maandalizi.

Chanzo: habarileo.co.tz