Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bilioni 34/kutumika Kagera kuunganisha umeme vijiji 114

Ad96e447f0a3712c7258f8ae61d43cde.jpeg Bilioni 34/kutumika Kagera kuunganisha umeme vijiji 114

Sun, 20 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

JUMLA ya Sh bilioni 34 zinatarajiwa kutumika kuunganishwa umeme katika vijiji 114 mkoani Kagera ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa kusambaza umeme vijijini kupitia kwa Wakala wa Umeme Vijijini (REA).

Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato alisema hayo wakati akizindua mradi wa REA awamu ya tatu mzunguko wa Pili katika Kijiji Cha Omurunazi Kata Mushabago, Wilaya ya Muleba.

Alisema miradi inayotekelezwa Sasa haitaacha viporo vya miradi iliyobaki katika REA zilizopita. Alisema kuna vijiji vilibaki katika miradi iliyopita hivyo wakandarasi wanapaswa kuhakikisha inatekelezwa.

Naibu waziri alisema kwa kutambua ucheleweshwaji wa vitongoji kupata umeme, Rais Samia Suluhu Hassan ameunda kitengo maalumu cha kuhakikisha umeme unashuka katika vitongoji kupitia Shirika la Umeme (Tanesco).

Mkoa wa Kagera umeshapokea Sh bilioni 25.5 kwa ajili ya kusambaza umeme katika vitongoji ambavyo havijafikiwa na umeme.

Mbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage alisema Wilaya ya Muleba ina visiwa vingi hivyo aliomba wizara kuongeza kasi ya kuwapatia wananchi wanaoishi visiwani umeme wa jua.

Chanzo: www.habarileo.co.tz