Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bilioni 3 kujenga madaraja Lulindi

15743 Pic+madaraja TanzaniaWeb

Thu, 6 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Jumla ya Sh 3.5 bilioni zinahitajika kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa madaraja ya Mwitika-Maparawe, Mipande-Mtengula na Mngangala-Mbuyuni wilaya ya Lulindi ambayo yalisombwa na maji.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Josephat Kandege ameliambia Bunge kuwa fedha hizo ni nyingi hivyo Tamisemi imeziweka katika fungu la maombi maalumu.

Kandege ametoa kauli hiyo bungeni leo Septemba 5, 2018 wakati akijibu swali la msingi la mbunge wa Lulindi Jerome Bwanausi (CCM).

Mbunge huyo alitaka kujua ni lini serikali itajenga madaraja hayo ili kuondoa adha ya usafiri inayowakabili wananchi.

Wakati huo huo Kandege amesema kiasi cha Sh22.6 bilioni zinatakiwa kujenga barabara ya Nzasa-Kilungure-Buza-Temeke pamoja na kuweka taa zitakazotumia umeme jua.

Naibu Waziri amesema tayari Sh 3.25 bilioni zimeshatengwa kwa ajili ya kulipa fidia wananchi 310 watakaopisha ujenzi huo.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz