Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bilioni 2/- kupelekwa kwa wakulima wa miwa Dodoma

34283c215f0c0b3e56432b579a358aaf Bilioni 2/- kupelekwa kwa wakulima wa miwa Dodoma

Fri, 4 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Mbunge wa Jimbo la Chamwino mkoani Dodoma, Deo Ndejembi (CCM) amewaahidi wakulima wa miwa jimboni humo kuwa yupo mbioni kuwaleta wafadhili watakaowekeza Sh bilioni mbili ikiwa ni hatua ya kuendeleza zao hilo.

Ndejembi ametoa ahadi hiyo alipokuwa katika Kata ya Dabalo mara baada ya kufanya kikao kifupi na wakulima hao ambapo aliambatana na wataalamu kutoka Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (TARURA) kwa lengo la kujionea changamoto za barabara ili waweze kuzirekebisha.

“Kuna wafadhili wameonesha nia ya kuwekeza shilingi bilioni mbili ikiwa ni hatua ya kuendeleza zao hilo ili waweze kufanya kilimo chenye tija na kunufaika,” alisema Ndejembi.

Chanzo: habarileo.co.tz