Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bilioni 2.1/- kukamilisha ujenzi wa daraja Morogoro

Fedhaa 0 Bilioni 2.1/- kukamilisha ujenzi wa daraja Morogoro

Thu, 10 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkandarasi anayejenga daraja la Kudumu la Luipa lililopo Mkoani Morogoro ametakiwa kuongeza kasi ili kukamilisha ujenzi wa daraja hilo kwa wakati.

Rai hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Mlimba, Godwin Kunambi wakati wa ziara yake katika jimbo hilo ambapo amekagua ujenzi wa hilo linalogharimu kiasi cha Sh Bilioni 1.2 ambalo litahudumia wananchi wa kata nne.

Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Mbunge Kunambi ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi huo utanufaisha wananchi wa kata hizo nne za Mbingu, Igima, Mofu na Namawala.

“Kukamilika kwa ujenzi huo utaepusha vifo vya wananchi hasa nyakati za mvua ambapo ilikua inashindikana kupitika kutokana na daraja la mbao lililokuepo kuzidiwa,” amesema Mbunge Kunambi.

Ameongeza kuwa daraja hilo litaboresha maisha ya wananchi wetu kiuchumi kwani sasa wataweza kusafirisha mazao yao bila changamoto yoyote ile.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live