Mbunge Jimbo la Chamwino, Dodoma na Naibu Waziri Tamisemi, Deo Ndejembi amesema Serikali imetenga kiasi cha Sh Bilioni 1.1 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya kuunganisha Kata ya Ikoa na Kata ya Manchali ambapo kinachosubiriwa ni kupatikana kwa mkandarasi ambaye atatekeleza kazi hiyo.
Ndejembi ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye mikutano ya hadhara na wananchi wa Kata hizo mbili katika muendelezo wa ziara yake ya kuzungumza na wananchi wa Jimbo hilo ambapo amefanya mikutano katika kata tatu za Msamalo, Ikoa na Manchali.
Siyo kwenye miundombinu tu, pia tumepokea Sh Milioni 544 za ujenzi wa shule ya pili ya Sekondari kwenye kata yetu na kama hiyo haitoshi, Rais Dkt Samia ametupatia tena Sh Bilioni 3 kwa ajili ya ujenzi wa Shule kubwa ya Wasichana kuanzia kidato cha kwanza hadi cha Sita ya Mkoa wetu wa Dodoma ambayo.
Aidha akiwa katika kijiji cha Makoja kata ya Ikoa, Ndejembi amewatoa hofu wananchi wa kijiji hicho kuhusu changamoto ya maji ambapo amewaeleza tayari zishapatikana Sh Milioni 30 za ujenzi wa kisima ambacho kitakua ni muarobaini wa changamoto hiyo ikiwa ni lengo la Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kumtua Mama Ndoo kichwani.