Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bila Barakoa hupati huduma hizi Dar es salaam

Barakoa Uvaaji wa Barakoa mkoani Dar es Salaam

Tue, 3 Aug 2021 Chanzo: Mwananchi

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amesema kuanzia sasa siyo hiari kuvaa barakoa bali ni lazima kwa watu wanaotumia usafiri wa umma au wanaokwenda au kuingia katika vituo vya mabasi.

Makalla ameeleza wakati akizungumza na wanahabari kuhusu mwenendo wa uchukuaji wa tahadhari kwa wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam.

Amesema wamefanya tathimini na kubaini kuna baadhi ya maeneo ikiwemo vyombo vya usafiri kuna ulegevu wa uchukuaji wa tahadhari.

Makalla ametoa msimamo huo, akiwa ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama wa Mkoa wa Dar es Salaam, akisisitiza kuwa ugonjwa wa corona upo na wagonjwa wapo katika hospitali za Serikali na binafsi , lazima wananchi waendelee kuchukua tahadhari za kujikinga.

"Ukiingia kwenye gari, kivuko lazima uvae barakoa, hili ni moja ya sharti. Nimefanya survey ukienda Kivukoni Feri mtu anaingia na barakoa kwa sababu ya usimamizi akiwa ndani anaivua, akitaka kutoka anaiva tena," amesema Makalla.

Pia Makalla amekazia suala la abiria kukaa kwenye daladala kulingana na idadi ya viti vilivyomo' level seat' akisema jambo hilo ni muhimu na wamiliki vyombo hivvyo vya usafiri kuanzia mwendokasi hadi daladala kulizingatia.

Kuhusu wanafunzi Makalla amesema lazima wavae barakoa wakati wa kutumia usafiri wa umma, huku akisema wao wataruhusiwa kusimama watano katika daladala akitaka utekelezaji huo ufanyike kikamilifu.

Chanzo: Mwananchi