Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bil 80/- kujenga majengo ya halmashauri 100

E1441fab3387d67a1500c2685ca0f3e4 Bil 80/- kujenga majengo ya halmashauri 100

Wed, 31 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

OFISI ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) katika kipindi cha Mwaka 2020/21 imetenga Sh bilioni 80.42 kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya utawala katika halmashauri 100 nchini.

Naibu Waziri Tamisemi, Dk Festo Dugange, alibainisha hayo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye (CCM) aliyetaka kujua ni lini ahadi ya Hayati John Magufuli na maagizo ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa yatatimizwa ili kuhakikisha ujenzi wa jengo la utawala katika halmashauri hiyo unakamilika.

Dk Dugange alisema hata katika bajeti ya mwaka 2021/22, Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya utawala katika halmashauri mbalimbali nchini.

Akijibu swali la Msingi la Mbunge wa Magu, Bonaventura Kiswaga (CCM) aliyetaka kujua serikali ina mpango gani wa kutoa fedha ili kukamilisha ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Magu, Dugange alisema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita Serikali imeendelea na ujenzi wa majengo ya utawala katika Halmashauri 75 ambazo zimegharimu Sh bilioni 147.33.

Alisema katika mwaka wa fedha 2021/22, serikali itaomba kutengewa Sh bilioni 83.75 ili kuendelea na ujenzi wa majengo ya utawala katika halmashauri nyingine 89.

Alisema, Serikali inaendelea na ujenzi wa jengo la utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Magu ambalo litagharimu Sh bilioni 5 hadi kukamilika.

Alisema hadi kufikia Februari 2021, Serikali ilikuwa imetoa Sh bilioni 3 kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo ambalo tayari limeezekwa.

Katika mwaka wa fedha 2020/21, Serikali imetenga Sh milioni 750 ili kuendelea na hatua ya ukamilishaji wa jengo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz