Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bil 23/- zajenga kituo cha umeme Morogoro

8935e7e00ff66952fbd8461e35836178.jpeg Bil 23/- zajenga kituo cha umeme Morogoro

Mon, 9 Aug 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

BODI ya Nishati Vijijini (REB), imeridhishwa na hatua ya ujenzi wa mradi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Ifakara mkoani Morogoro unaogharimu Sh bilioni 23.

Fedha hizo zinatolewa kwa pamoja kati ya Serikali ya Tanzania na Umoja wa Ulaya (EU).

Mwenyekiti wa REB, Julius Kalolo, alisema hayo mjini Ifakara wilayani Kilombero, wajumbe wa bodi walipotembelea miradi miwili ya ujenzi wa kituo hicho kwa ajili ya kujionea shughuli zinazoendelea na utekelezaji wa maagizo ya awali ya bodi.

Kalolo alisema katika mradi huo lazima wataalamu wawepo kituoni ili kusimamia shughuli za kila siku.

Aliagiza mameneja hao waongeze idadi ya wafanyakazi ili kazi zifanyike usiku na mchana, hali itakayowezesha mradi kukamilka Mei, mwakani.

Kalolo alitaka wataalamu watoe taarifa kwenye bodi kuhusu maendeleo ya mpango kazi kila wiki sanjari na kukutana mara kwa mara kwa kushirikiana na wadau likiwemo Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), na Wakala

wa Nishati Vijijini (REA) ngazi ya wilaya na mkoa.

Mkurugenzi Mkuu wa REA, Amos Maganga, alisema jukumu la wakala huo ni kuhakikisha nishati ya umeme inawafikia wananchi wote vijijini na mijini.

Maganga alisema ifikapo Septemba mwaka huu kazi zote zilizopo zitakuwa zimekami-

lika na transfoma ambazo ni vifaa vikubwa katika mradi huo zitaletwa kwenye eneo la mradi ifikapo Novemba 24, mwaka huu.

Meneja Mradi wa Ujenzi wa Kituo hicho, Francis Kahumbi, alisema kazi inaendelea na wataikamilisha ndani ya wakati kwa mujibu wa mkataba.

Kahumbi alisema kwa sasa mradi umefikia hatua nzuri na hadi Novemba mwaka huu, utafikia asilimia 50 na kazi itakayobakia itakuwa ni kuweka vifaa vya umeme.

Meneja Mradi Ifakara kutoka Tanesco, Didas Lyamuya, alisema mradi huo mpaka sasa ujenzi wake umefikia asilimia 30.

Chanzo: www.habarileo.co.tz