Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bil 13.88/- zatengwa ukarabati wa barabara Geita

Fe2d7a7cd2cbc0908faa87df34342c34 Bil 13.88/- zatengwa ukarabati wa barabara Geita

Mon, 22 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WAKALA wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) Mkoa wa Geita wametenga Sh bilioni 13.88 kwa ajili ya ukarabati wa barabara mkoani hapa.

Hayo yalisemwa wakati wa kikao cha majadiliano ya maendeleo ya barabara kilichohusisha viongozi wa halmashauri zote, majimbo na wadau wote wa maendeleo ya barabara mkoani Geita.

Meneja wa Tanroads Mkoa wa Geita, Harun Senkunku alisema kwa upande wao wametenga takribani Sh bilioni 13.08 kwa ajili ya kufanyia ukarabati barabara ili ziendelee kupitika kwa mwaka mzima.

Kwa upande wake Meneja wa Tarura Mkoa wa Geita, Chacha Moset alisema taasisi hiyo imepanga bajeti ya Sh milioni 800 ili kufanyia ukarabati maeneo yenye changamoto ya miundombinu ya barabara zilizo chini ya usimamizi wa Tarura.

"Tarura Mkoa wa Geita inaendela kufanyia kazi malalamiko yote ya changamoto za miundombinu ya barabara na maeneo mengine tumeshaanza kufanyia marekebisho na maeneo mengine tunatarajia kuanza utekelezaji hivi punde ikiwemo Mbogwe na Nyanghwale," alisema.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel aliwataka Tanroads na Tarura mkoani hapa kuongeza umakini katika utekelezaji wa majukumu yao.

Aidha Gabriel alizitaka halmashauri zote mkoani hapa kutenga bajeti ya dharura ya ukarabati wa barabara na kuwasisitiza wahandisi wanaohusika kukutana nyakati za mvua na kufanya tathimini ya ukarabati imara kuepuka matengenezo ya mara kwa mara.

Chanzo: habarileo.co.tz