Ujenzi wa barabara zinazoelekea katika maeneo ya Mgodi Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi katika Mwaka wa fedha wa 2021/2022 zaidi ya shilingi bilion kumi na moja zimetumika kugharamia shughuli hiyo.
Hayo yamebainishwa Jana na Meneja waTarura Wilaya ya Ruangwa Mhandisi Mashaka Narubi, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya madini yanayoendelea katika wilaya ya Rwangwa ambapo amesema kuwa pia mwaka huo huo wa fedha 2021/2022 wamejenga barabara za lami maeneo ya mji wa Rwangwa mjini ambazo zinaelekea maeneo yote ya migodi ambapo zimegharimu shilingi bilioni 5.2.
Amesema lengo la ujenzi wa barabara hizo ni kurahisisha shughuli za uchimbaji wadini unaoendelea Wilayani humo ili ziweze kupitika katika kipindi chote cha mwaka.
"Kwenye mpango wetu wa mwaka 2021 mpaka mwaka 2023 tumejengaa jumla ya madaraja madogo 47 ambapo shilingi bilion 1.5 zilitumika katika ujenzi huo na nadaraja yotectuliyoyajenga maeneo ya vijijini ambapo kama fusa kwa wachimbaji wetu wa madini"amesema Mhandisi mashaka.
"Mwaka huu wa fedha 2023/2024 tunakusudia kujenga barabara kilomita 110 kuelekea maeneo ya madini ambapo tunatarajia kutumia bilion 3.4 kwa ajili ya barabara katika maeneo ya madini"ameongeza.
Pia amesema Tarura Wilaya ya Rwangwa imejilita zaidi kuboresha barabara zinazoelekea kwenye maeneo yenye fursa ya madini ambapo wanaamini kwakufanya hivyo wawekezaji wa madini wajitokeza kwa wingi wilayani humo.
Mhandisi Mashaka ameongeza kuwa mbali na kujenga barabara hizo pia wana mpango wakuongeza barabara nne ambazo zinaelekea kwenye maeneo kwenye maeneo ya madini kwa kiwango cha lami kutoka Rwangwa kuelekea eneo la Nangurugai ambapo kuna mgodi wa grafact ambapo amesema amesema wameshaanza usanifu na mwezi wa kumi mwaka huu taanza ujenzi wake ambao itakuwa kilometa thelathini na moja.
"Tuna mpango wa kuongeza barabara nne ambazo zinaelekea kwenye maeneo kwenye maeneo ya madini kwa kiwango cha lami kutoka Rwangwa kuelekea eneo la Nangurugai ambapo kuna mgodi wa grafact ambapo tumeshaanza usanifu na mwezi wa kumi mwaka huu tanaanza ujenzi huu, ambao itakuwa kilometa thelathini na moja" amesema Mhandisi Mashaka.