Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bil 1.4 zatengwa daraja la Mihyunge- Serikali

7ad95f393c1c30635e5e95413345899b Bil 1.4 zatengwa daraja la Mihyunge- Serikali

Wed, 21 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SERIKALI imetenga Sh bilioni 1.4 kwa ajili ya ujenzi wa daraja la Mihyunge wilayani Ikungi.

Akizungumza Bungeni leo Naibu Waziri Wizara ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) David Silinde alisema mbali na fedha hizo za ujenzi wa daraja pia serikali imetenga Sh milioni 925.8 kwa ajili ya matengenezo ya barabara zenye urefu wa kilomita 92.6.

Silinde alisema hayo akijibu swali la Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu aliyehoji ni lini Serikali itatekeleza maelekezo ya Waziri Mkuu ya ujenzi wa barabara ya urefu wa kilomita tano kwa kiwango cha lami Wilayani Ikungi.

Silinde alisema katika Mwaka wa Fedha 2021/22, Serikali kupita Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imepanga kufanya usanifu na tathmini ya gharama za ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha lami katika Mji wa Ikungi.

Alisema utambuzi wa barabara hizo utakuwa shirikishi ili kutoa kipaumbele kwenye barabara zenye umuhimu mkubwa.

“Hadi kufikia Machi 2021, TARURA imetoa shilingi milioni 598.22 kati ya Shilingi milioni 890.89 zilizotengwa kwa ajili ya matengenezo ya barabara zenye urefu wa kilomita 97.92 katika ya Wilaya ya Ikungi,”alisema

Aidha, alisema katika Mwaka wa Fedha 2021/22, Serikali itaomba kuidhinishiwa Shilingi milioni 925.08 kwa ajili ya matengenezo ya barabara zenye urefu wa kilomita 92.6 na vile Shilingi bilioni 1.4 zitatengwa kwa ajili ya ujenzi wa daraja la Mihyuge Wilayani Ikungi.

Alisema kwa sasa serikali inafanya tathmini na usanifu wa barabara za kilomita tano ikiwemo ya Ikungi ambapo Mwaka wa Fedha wa 2021/2022 Tarura itatenga fedha kwa ajili ya barabara hizo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz