Mwanaiba Omary mwenye umri wa zaidi ya miaka 90 mkazi wa mtaa wa Mloweka kata ya Lizaboni manispaa ya Songea mkoani Ruvuma amemuomba Rais wa Tanzania Samia Hassan Suluhu Hassan amsaidie kuipata nyumba yake
Hiyo ni baada ya baraza la ardhi la wilaya ya Songea kutoa amri ya siku 45 aondoke kwenye nyumba hiyo baada ya mtoto wake kushinda kesi ya umiliki wa nyumba hiyo
Bi Mwanaiba Omary ni mzee mwenye umri wa zaidi ya miaka 90 na ni mkazi wa mtaa wa Mloweka kata ya Lizaboni manispaa ya Songea mkoani Ruvuma na ni mjane amebahatika kuwa na watoto wawili wakike
Anasema baada ya mume wake kufariki alimuachia nyumba ambayo ukarabati wake haukumalizika na yeye aliiuza nyumba hiyo na kununua nyumba nyingine ambayo ameishi na familia yake kwa muda mrefu
Anasema ameshangaa sasa binti yake wa mwisho anadai kuwa nyumba ni ya kwake na kisha binti huyo akafungua kesi baraza la ardhi la wilaya ya Songea na akafanikiwa kushinda kesi hiyo
Kwa sasa bibi huyo amepewa siku 45 awe ameondoka kwenye nyumba hiyo ambayo yeye anaamini hajatendewa haki ya kunyang'anywa nyumba hiyo anasema kuwa binti yake ametumia fedha kushinda hiyo kesi sasa anaiomba serikali kuingilia kati na anamuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Hassan Suluhu Hassan amsaidie kuipata nyumba yake.