Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bibi aua wajukuu zake wanne kwa moto wa petroli akiuwa kunguni

Moto Manya Bibi aua wajukuu zake wanne kwa petroli akiuwa kunguni

Sat, 7 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watoto 4 waliokuwa wakiishi na bibi yao wamefariki dunia kwa ajali ya moto katika Kitongoji cha Ndeves kilichopo Kijiji cha Ngage, Kata ya Lobosoi (B) wilayani Simanjiro mkoani Manyara huku chanzo kikidaiwa kuwa ni bibi huyo kuua kunguni kwa kutumia mafuta ya petroli.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara, ACP Benjamin Kuzanga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema biibi huyo aitwaye Anna Kiputu (61) mkazi wa Kitongoji cha Ndeves akiwa nyumbani kwake pamoja na wajukuu zake hao walikumbwa na tukio hilo baada ya nyumba yao kuungua kwa moto kufuatia bibi huyo kutumia mafuta ya petroli kuua kunguni.

Kamanda Kuzanga amesema tukio hilo limetokea Mei 3, 2022 majira ya saa 8 mchana. ACP Kuzaga amewataja walio fariki katika tukio hilo kuwa ni Sifa Mathayo (6), Jackson Mathayo (5), Sioni Raphael (4), Napokei Raphael (7) huku Bibi huyo akiwa katika hali mbaya na kukinbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC iliyopo Moshi Mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya matibabu zaidi.

Aidha, Kamanda Kuzaga ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanaokata ushauri kwa wataalamu wa mifugo ili kuweza kupata dawa sahihi za kuua wadudu kama vile viroboto na kunguni katika familia ikiwa ni namna sahihi ya kukabiliana wa wadudu hao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live