Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bibi anyongwa hadi kufa na wanae, sababu zawekwa hadharani

FEDHA WEB Bibi anyongwa hadi kufa na wanae, sababu zawekwa hadharani

Wed, 15 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bibi mwenye umri miaka 80, Fatuma Kimbawala, Mkazi wa Mtaa wa Magongo Halmashauri ya Mji wa Makambako Mkoani Njombe ameuawa kwa kunyongwa kisa mali huku Watoto wake wanne wakikamatwa kwa kuhusishwa na tukio hilo.

RPC wa Njombe, Hamis Issah amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akiwataka Wananchi Mkoani Njombe kutumia Vyombo mbalimbali vilivyo sahihi ili kupata ufafanuzi juu ya mgawanyo wa mali.

"Watoto wa huyu Mama tumewakamata baada ya kuhusishwa na tukio la huyu Mama, bado kuna maswala ya kugombania mali za urithi kwenye Jamii Mkoani Njombe, tunawaomba Wananchi kama kuna mali inagombewa kuna Vyombo ambavyo vinaweza kutumika"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live