Bibi mmoja anayefahamika kwa jina Vestina Joeli katika mtaa wa Uwanja Kata ya Nyankumbu wilayani Geita amemuunguza mtoto (jina limehifadhiwa) mikono yake kwa madai kuwa ameiba karanga za mboga maarufu kama Kitwiri.
Akiwa anaugulia maumivu makali mtoto huyo amesema bibi yake alimpeleka jikoni na akaweka mikono yake kwenye mafiga ya kupikia na kuanza kumuunguza na moto huku akisema mototo huyo aache tabia ya udokozi.
Bibi huyo amekiri kufanya kitendo hicho kwasababu ya hasira na hakufikiria kwamba kitendo alichokifanya kingeleta madhara makubwa kwa mototo huyo.
Mwenyekiti wa mtaa, Enos Chelehani amethibitisha kupokea taarifa za tukio hilo la mototo kuunguzwa mikono na bibi yake kwa kosa kudokoa karanga za mboga na kwamba bibi huyo atafikishwa polisi kwa hatua za kisheria zaidi.